Mungu Hakopeshwi

£51.98

Mungu Hakopeshwi

Modern and contemporary fiction: general and literary

Dinosaur mascot

Language: English

Published by: Mkuki Na Nyota Publishers

Published on: 2nd June 2023

Format: LCP-protected ePub

ISBN: 9789987449286


Riwaya ya Mungu Hakopeshwi

Inaelezea maisha ya familia moja ya Unguja iliyoingia katika mitafaruku na mikasa mingi. Kila kitu huwa na chanzo na khatima; basi ni nini chanzo cha mitafaruku hiyo na khatima yake ilikuwaje?

Simulizi ni juu ya baba, Bw. Ahmed, mwenye hasira kali zisizo na mipaka, aliyeongoza familia yake kwa utashi wa nafsi yake, bila kujali hisia za mkewe wala wanawe. Kumbe moyoni mwake alihifadhi siri, na hiyo siri ndiyo iliyomfanya Bw. Ahmed kuwa mkali bila kiasi, ikimsukuma azuie kurejea kwa yale yaliyomfika zamani.

Lakini kivuli cha historia ya maisha yake ya nyuma hakikuacha kumuandama. Riwaya hii imeandikwa kwa lugha nzuri na fasaha, kwa ufundi wa msanii makini na mwelewa wa maisha ya jamii za Kizanzibari na za mwambao kwa jumla.

Show moreShow less